Lukuvi atoa changamoto – Wakurugenzi wa manispaa na madiwani wametakiwa kuharakisha utungaji wa sheria ndogo ili kufanikisha mpango mkakati wa kuboresha mazingira na usafi wa jiji. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Milliam Lukuvi, aliyasema hayo juzi ofisini kwake, wakati akipokea mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya kuboresha mazingira na usafi wa jiji. Alisema kutungwa kwa sheria hizo, kutasaidia kuboresha hali ya usafi wa jiji, ambalo kwa sasa ni chafu. “Jiji ni chafu sana na kunahitajika hatua za haraka za kupambana na hali hiyo, hivyo mapendekezo ya kamati yanatakiwa kufanywa kazi haraka sanana manispaa zoe” aliseama Lukuvi.